Instance Results

Topics:kuteswa+na+kufa+kwa+yesu
In:instances

Planning worship? Check out our sister site, ZeteoSearch.org, for 20+ additional resources related to your search.
Showing 1 - 10 of 24Results Per Page: 102050
TextPage scan

Yesu, kuteswa kwako

Author: S. V. Birken, 1626-1681 Hymnal: Mwimbieni Bwana #82 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Yesu, kuteswa kwako nitakufikiri. Nipe kwa shauri hili roho na mbaraka. Moyo wangu uone hali yako Yesu, jinsi ulivyoteswa kwa ajili yetu. 2 Moyo wangu uone taabu yako kubwa, maumivu, mapigo, na kuwambwa mtini, taji lako la miiba tena misumari, iliyokuumiza, hata kufa kwako. 3 Nikitazama yote yaliyokutesa, nifikiri sababu na maana yake. Sababu ndio mimi na makosa yangu: umepata mateso, nipate huruma. 4 Yesu unifundishe nijute kwa moyo; nisikuzidishie shida na uchungu. Nisiweze kupenda yaliyokutesa: nataka kuyaacha na kukufuata. Languages: Swahili
TextPage scan

Nakusalimu kichwa

Author: Bernhard V. Clairvaux, 1091-1153; Paul Gerhardt, 1607-1676 Hymnal: Mwimbieni Bwana #78 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Nakusalimu kichwa kilichojaa damu, kilichovikwa taji la miiba mikubwa, kilichopata enzi kwa Mungu mbinguni, kitukanwacho sasa matusi makali. 2 Naona uso wako watemewa mate, heshima yako yote imeondolewa. Mwanga wa macho yako wazimika sasa. Aliyekuharibu hivi, ndiye nani? 3 Mateso yako Bwana, yanipasa mimi. Wewe waadhibishwa kwa ajili yangu. Hukumu unapata iliyonipasa. Bwanangu nakuomba, unihurumie! 4 Na mimi nasimama msalabani pako; niwe karibu kwako utoapo roho; ukiugua sana kwa teso la kufa, nitakushika Bwana kwa moyo wa pendo. 5 Bwana nayashukuru masumbaku yako, sababu ya kuteswa na kufa kuchungu. Wewe umenishika, nami nakushinka, mwisho nitakufia uliyenifia. 6 Moyo unaposhikwa na woga wa kufa, usiniache Bwana katika vita hii. Siku ya kufa kwangu unisaidie, kufa kwako kuchungu kutaniokoa. 7 Niwie kama ngao nitakapokufa, nione uso wako katika uchungu. Ndipo nikutazame nikukumbatie! Anayekufa hivi afa kwa amani. Languages: Swahili
TextPage scan

Nataka kusimama

Author: E. C. Clephane, 1830-1869 Hymnal: Mwimbieni Bwana #87 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Nataka kusimama chini ya msalaba, kama kivuli cha mwamba wakati wa mchana, kama ni maji nyikani, kambi safarini, na hapa nitapumzika, kwani jua kali. 2 Mahali pema sana chini ya msalaba, kwani hapo waoneka upendo wa Yesu. Yakobo alivyoona ndotoni zamani, mti Yesu aliowambwa, ni ngazi kwa Mungu. 3 Juu ya msalaba huo Yesu alikufa. Alikufa tuokoke, tuliopotea. Ninastaajabu kabisa ni mambo mawili: kwake Yesu ni upendo, kwangu mimi kosa! 4 Wataka kuonana na Yesu mbinguni, yakupasa kukaa kwanza chini ya mti huo. Ni kweli siku chache tu mateso na shaka. Halafu pasipo mwisho furaha kwa Bwana! Languages: Swahili
TextPage scan

Nimshangilie Bwana wangu

Author: Ph. Bliss Hymnal: Mwimbieni Bwana #83 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Nimshangilie Bwana wangu na kumwimbia mkombozi, katukomboa msalabani, nisifu pendo lake kuu. Haya mwimbieni Yesu, amekubali mateso, katukomboa msalabani, tusifu pendo lake kuu! 2 Tumsifu yeye mponya wetu katika ulimwengu huu, kutupatanisha na Baba walio wakosaji tu. Haya mwimbieni Yesu, amekubali mateso, katukomboa msalabani, tusifu pendo lake kuu! 3 Katuletea mwanga wake, tulikaa katika giza, wokovu ukaonekana, kamshinda mwovu, ni shujaa! Haya mwimbieni Yesu, amekubali mateso, katukomboa msalabani, tusifu pendo lake kuu! 4 Na tumtukuze Bwana wetu, tumtumikie kwa bidii, na atawale apendavyo, na sisi sote tutamtii! Haya mwimbieni Yesu, amekubali mateso, katukomboa msalabani, tusifu pendo lake kuu! Languages: Swahili

Wakristo twabeba nini?

Author: Z. D. Mzengi Hymnal: Mwimbieni Bwana #95 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Languages: Swahili
TextPage scan

Ee, watoto njooni

Author: E. G. Woltersdorf Hymnal: Mwimbieni Bwana #86 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Ee, watoto njooni, njooni Golgota, mtazameni Yesu aumizwavyo! 2 Mtazameni huko mkamtazame, Sogeeni kwake, ametupenda. 3 Sogeeni kwake, mkamtazame, mioyo iyevuke, mwangukieni! 4 Mioyo imlilie anayeteswa; mzigo wetu mkubwa aukubali. 5 Mzigo wa makosa ya ulimwengu. Mpeni nanyi nyote mioyo yenu! 6 Apata mshahara, ni kufa kwake; wewe una raha, kwake ni kufa. 7 Ataona enzi ya utukufu. Tuimbe Haleluya na kumshukuru! Languages: Swahili
TextPage scan

Mwokozi wangu umekosa nini

Author: J. Heermann, 1585-1647 Hymnal: Mwimbieni Bwana #77 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu First Line: Mwokozi wangu, umekosa nini? Lyrics: 1 Mwokozi wangu, umekosa nini? Wahukumiwa kama mwuaji. Umeshtakiwa makosa mangapi uliyotenda? 2 Wapigwa sana, miiba taji lako, umetemewa mate, watukanwa, wanyweshwa nyongo, tena siki kali, wasulibishwa! 3 Sababu gani unateswa hivi? Makosa yangu yanakuumiza; mateso haya yako yanipasa, mimi mkosaji. 4 Ajabu kubwa sana tendo lako: Mchungaji unateswa kwa ajili ya kondoo, Bwana unawalipia watumwa wako. 5 Tulipokuwa mateka ya mwovu, nawe ukaja ukatukomboa. Twalistahili kufa kwa milele, ukatufia. 6 Mwokozi wangu nifanyeje mimi, niitangaze pote sifa yako? Nakufuata nikutumikie maisha yote. Languages: Swahili
TextPage scan

Roho yangu tua hapa

Author: G. Tersteegen, 1697-1769 Hymnal: Mwimbieni Bwana #85 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Roho yangu tua hapa mlimani pa Golgota, angalia tendo hili, afanyalo mfalme mkuu. Amevutwa na upendo kuacha enzi yake. 2 Yesu alivyotupenda, twaona msalabani, maumivu hata manza ya makosa yampata. Anakaa malali petu, sikia ateswavyo! 3 Kufa kwako kunivute nife pamoja nawe, mwili na mapenzi yangu yakazikwe nawe. Niwe na kutengemana, mwenye pendo la kweli! Languages: Swahili
TextPage scan

Ulimwengu tazama

Author: Paul Gerhardt, 1607-1676 Hymnal: Mwimbieni Bwana #80 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Ulimwengu tazama, Yesu Mwokozi wako asulibiwavyo. Mwenye heshima yote anayavummilia mateso tena matusi. 2 Karibia tazama maungo yake yote yatokavyo damu. Na moyo wake mwema kwa shida na uchungu unaugua vigumu. 3 Nani akupigaye, aliyekufanyia mambo kama haya? Wewe huna makosa kama wengine wote, hujui kosa lolote. 4 Makosa yangu mimi yaliyo kama mchanga, hayahesabiki, ndiyo yakutiayo mateso na uchungu uliyoyavumilia. 5 Mimi nimestahili kulipa haya yote, na kufungwa sana. Mapigo na mateso uliyopata wewe yalitoka kwangu mimi. 6 Umejitwika mzigo ulio mzito sana kuliko jiwe kuu. Wachukua maovu, tupate kuokoka tukae nawe daima! Languages: Swahili
TextPage scan

Liko neno moja nipendalo

Author: A. Kanpp, 1798-1864 Hymnal: Mwimbieni Bwana #79 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Liko neno moja nipendalo, ni chakula cha moyo; neno hili linanituliza nikipatwa na shida: Kumtazama Bwana wetu pale, atoapo jasho kama damu, akubalipo mzigo, Baba aliomtwika. 2 Siku zote namkumbuka yeye, alivyosulibishwa, akivumilia taabu kimya kama mwana wa kondoo. Nami akanikumbuka mimi, akisema: Yamemalizika! Huko aliniteka, nami niwe mtu wake. 3 Bwana wangu, u mwenye huruma, mimi ni mkosaji tu; nilipokuwapo penye giza wewe ukatokea, ukamtafuta kondoo wako, kabla mimi sijakusikia. Watoa makombozi yanipayo uhuru. 4 Nimi huru lako, Bwana Yesu, wewe ndiwe Bwanangu. Jina lako, bora liung'aze moyo wangu vizuri. Amani yako tukae nayo, siku zangu zote mpaka kufa. Ndivyo ninavyoomba, Bwana unikubali. Languages: Swahili

Pages


Export as CSV