79. Liko neno moja nipendalo

1 Liko neno moja nipendalo,
ni chakula cha moyo;
neno hili linanituliza
nikipatwa na shida:
Kumtazama Bwana wetu pale,
atoapo jasho kama damu,
akubalipo mzigo,
Baba aliomtwika.

2 Siku zote namkumbuka yeye,
alivyosulibishwa,
akivumilia taabu kimya
kama mwana wa kondoo.
Nami akanikumbuka mimi,
akisema: Yamemalizika!
Huko aliniteka,
nami niwe mtu wake.

3 Bwana wangu, u mwenye huruma,
mimi ni mkosaji tu;
nilipokuwapo penye giza
wewe ukatokea,
ukamtafuta kondoo wako,
kabla mimi sijakusikia.
Watoa makombozi
yanipayo uhuru.

4 Nimi huru lako, Bwana Yesu,
wewe ndiwe Bwanangu.
Jina lako, bora liung'aze
moyo wangu vizuri.
Amani yako tukae nayo,
siku zangu zote mpaka kufa.
Ndivyo ninavyoomba,
Bwana unikubali.

Text Information
First Line: Liko neno moja nipendalo
Title: Liko neno moja nipendalo
German Title: Eines wünsch ich mir vor allem andern
Author: A. Kanpp, 1798-1864
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Kuteswa na kufa kwa Yesu
Notes: Sauti: Herr und Älster deiner Kreuzgemeine, Asili: Herrnjut 1759, Nyimbo za Kikristo #61, Wimbo: Posaunen Buch, Erster Band, #19
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us