1 Liko neno moja nipendalo,
ni chakula cha moyo;
neno hili linanituliza
nikipatwa na shida:
Kumtazama Bwana wetu pale,
atoapo jasho kama damu,
akubalipo mzigo,
Baba aliomtwika.
2 Siku zote namkumbuka yeye,
alivyosulibishwa,
akivumilia taabu kimya
kama mwana wa kondoo.
Nami akanikumbuka mimi,
akisema: Yamemalizika!
Huko aliniteka,
nami niwe mtu wake.
3 Bwana wangu, u mwenye huruma,
mimi ni mkosaji tu;
nilipokuwapo penye giza
wewe ukatokea,
ukamtafuta kondoo wako,
kabla mimi sijakusikia.
Watoa makombozi
yanipayo uhuru.
4 Nimi huru lako, Bwana Yesu,
wewe ndiwe Bwanangu.
Jina lako, bora liung'aze
moyo wangu vizuri.
Amani yako tukae nayo,
siku zangu zote mpaka kufa.
Ndivyo ninavyoomba,
Bwana unikubali.
Source: Mwimbieni Bwana: msifuni Mungu, mfalme wa mbingu na nchi! #79